Rhett Ayers Butler, mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika la Mongabay, ametajwa kwenye Orodha ya Viongozi wa Endelevu katika jarida la Forbes mwaka wa 2025, orodha inayowaheshimishia zaidi viongozi 50 wa kimataifa wanaofanya kazi ili kukabiliana na mzozo wa hali ya hewa.
“Mongabay imekuwa na uzoefu wa kusalia chini ya umaarufu. Tumezingatia uandishi wa habari badala ya kujitangaza wenyewe, hivyo utambuzi huu ni wa maana sana, na unaonyesha michango ya kila mtu anayehusika,” Butler alisema.
Utambuzi huo ni hatua muhimu iliopigwa katika safari ambayo inarudi nyuma kama miaka 25 hadi wakati Butler alipokuwa kijana akizuru msitu wa mvua huko Borneo.
“Nakumbuka vyema nikipoesha miguu yangu kando ya kijito cha msituni wakati orangutan wa mwituni alipoibuka kwenye dari. Tuliangaliana macho kwa macho, kwa sekunde chache, lakini muda huo ulisalia nami,” aliiambia Forbes.
Baadaye aligundua kwamba msitu aliokuwa na uzoefu nao mkubwa ulipaswa kuharibiwa kwa ajili ya mashapo na karatasi. Habari hizo za kuhuzunisha zilimchochea kujitolea katika maisha yake yote kujihusisha na uhifadhi; hatimaye aliacha kazi yake ya ufundi wa teknolojia huko Silicon Valley na kuanzisha shirika la Mongabay nje ya nyumba yake ya California.
“Wazazi wangu hawakufurahishwa na wazo hilo,” akakumbuka. “Mara nyingi niliulizwa ni lini nitapata ‘kazi halisi.’ Ilimchukua miaka kadhaa na utambuzi wa nje kwao kuona kwamba Mongabay inaweza kuwa ‘kazi halisi.’
Leo hii, shirika la Mongabay ni chumba cha habari cha kimataifa chenye takriban wachangiaji 1,000 kwenye zaidi ya nchi 80, kikizalisha vipindi vya podikasti, makala ya video na makala mingineo katika lugha saba kutoka ofisi za Marekani Kusini, India, Afrika na Brazil. Mamia ya vyombo vya habari vya mataifa hayo huchapisha upya maudhui ya Mongabay, ulimwenguni kote.
Shughuli hizo zote, upanuzi na uhamasishaji ni katika kuhudumia lengo moja: “kuhakikisha kwamba taarifa za ukweli za mazingira zinapatikana kwa kila mtu, hususan kwa wenye uwezo wa kuchukua hatua,” Butler aliiambia Forbes.

Tofauti na vyombo vingi vya habari, Mongabay haipimi mafanikio yake kwenye kubonyeza au kutembelea ukurasa wa tovuti yake. Badala yake, inazingatia “matokeo ya maana, ya dunia halisi,” Butler aliongeza.
Kwa sababu hiyo, shirika lajihusisha moja kwa moja na watengezaji wa sera na jamii za mashinani zilizoathiriwa na uharibifu wa mazingira. Mpango wa Mongabay wa kubadilisha hadithi ulioratibiwa, kwa mfano, utatumia akili bandia (yaani AI), pamoja na wahariri wa binadamu kupanga upya ripoti asili katika lugha za sauti na za jamii kwa jamii zilizoko kwenye mstari wa mbele ambazo zinaweza kutatizika na vizuizi katika ufikiaji, lugha au kusoma na kuandika.
Ushirikiano wa moja kwa moja wa shirika la Mongabay umezalisha athari chanya zinazoonekana sehemu za mashinani. Nchini Gabon, utangazaji wa mapambano ya jamii dhidi ya kampuni ya kigeni ya kukata miti ulisaidia kusababisha kufutiliwa mbali kwa kibali cha kampuni hiyo, mara ya kwanza kutokea nchini Gabon.
Kuripoti kutoka Paraguay kulihusisha ukataji miti haramu na ng’ombe na ngozi, na kusaidia kushinikiza Jumuiya ya Ulaya (EU) kujumuisha ngozi katika sheria yake ya kupinga ukataji miti.
Nchini Peru, ripoti ya shirika la Mongabay kuhusu shughuli za United Cacao ilichangia serikali kubatilisha kibali chake, kampuni hiyo kuondolewa katika Soko la Hisa la London na ulinzi wa karibu hekta 100,000 za msitu wa mvua.
“Haya si mafanikio yaliofichika tu, ni misitu ambayo bado imesimama, jamii zilizowezeshwa na mifumo ikolojia kupewa fursa ya pili. Kuwa na ushahidi kwa vitisho na uwezekano kunanikumbusha kila siku kwamba kusimulia taarifa hizi ni muhimu,” Butler alisema.
Picha ya bango: Rhett Butler katika Amazon ya Ekuador. Picha na Rhett A. Butler/Mongabay
Habari hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza hapa kwa lugha ya Kiingereza mnamo tarehe 19/09/2025