- Maelfu ya makazi nchini Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yategemea Ziwa Albert kwa mahitaji yao ya kila siku ya maji na samaki, na hutoa makazi muhimu kwa wanyamapori wa kipekee kama vile korongo na Nguli wa Goliath.
- Viwanja viwili vya mafuta – Kingfisher katika ufuo wake wa mashariki na Tilenga karibu na kituo cha kaskazini-mashariki cha Ziwa Albert – katika maendeleo yanayoendelea huko, na mshirika wa Uganda wa kampuni ya China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) na Total E&P Uganda, mtawalia, inaonekana kuwa tishio kwa ubora wa maji na wanyamapori, maoni mapya yanabishana.
- “Matatizo kama kutojitolea kwa mfumo wa utupaji maji, maji taka, na vipandikizi vya kuchimba visima yote yanaonyesha ishara mbaya katika eneo ambalo ni makazi ya wanyamapori wa kipekee,” mwandishi anaandika.
- Chapisho hili ni maoni. Maoni yaliyotolewa ni ya mwandishi, sio lazima ya Mongabay.
Hofu ya kuwekeza kwa uchache kukabiliana na kuvuja kwa mafuta, utupaji duni wa taka na matumizi ya maji kupita kiasi bado ni tatizo kubwa kwa wanamazingira, ingawa Uganda inasisitiza kuwa kuna hatua za kutosha kulinda Ziwa Albert na mfumo ikolojia unaozunguka kutokana na athari mbaya za uchimbaji na maendeleo ya mafuta ya petroli.
Ripoti iliyoagizwa na shirika langu, Watetezi wa Mazingira – shirika la uhifadhi na haki za binadamu linalojitolea kulinda bayoanuwai na haki za jamii asili- inapata kuwa uharibifu wa viumbe hai, umwagikaji na uchafuzi wa maji ya chini ya ardhi ni matukio yanayoendelea kujitokeza katika eneo la Albertine.
Ripoti hiyo inasutumu zaidi utundikaji wa vifaa vya uchimbaji mafuta kwenye mwambao wa Ziwa Albert bila uwekezaji wa kutosha katika hatua za kukabiliana na maeneo ya Tilenga na Kingfisher. Kulingana na ripoti hiyo, zinaleta vitisho vikubwa kwa mazingira, maji na afya ya jamii zinazozunguka ziwa hilo.

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), takriban makazi 100,000 yategemea Ziwa Albert kukidhi mahitaji yao ya maji, na zaidi ya watu 20,000 huvua na kula samaki kutoka katika ziwa hilo. hivyo, kuna hofu kwamba umwagikaji mkubwa wa mafuta ungeweza kutishia uwepo wa jamii hizi, ila upunguzaji dhidi ya tukio kama hilo haujatosha.
Kampuni ya kimataifa ya E-Tech awali ilithibitisha kwamba teknolojia inayotumika katika eneo la Albertine inalenga kuongeza faida na wala sio kulinda mazingira. Kulingana na ripoti hio, lengo la kutumia teknolojia ya bei nafuu ili kuongeza faida ni hatari, ikizingatiwa kwamba visima 10, kilomita 181 za bomba na miundombinu ya barabara zitawekwa katika Hifadhi ya Kitaifa ya Murchison Falls iliyo karibu.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mbuga hiyo inatumika kama makazi ya wanyamapori wanaozidi kuwa adimu ambao hawawezi kuishi pamoja na shughuli za ukuzaji mafuta. Kwa sababu ina aina mbalimbali za mimea na wanyama, Mbuga ya Kitaifa ya Murchison Falls inahitaji utunzaji mairi, ambao mwandishi wake anapendekeza kuwa unaweza kufanikiwa kupitia uajiri wa teknolojia bora zaidi inayopatikana.

Kwa mfano, mwandishi wa ripoti ya kampuni ya kimataifa ya E-Tech anapendekeza kupunguzwa kwa visima vya mafuta vya Tilenga kutoka 10 hadi viwili vilivyowekwa vizuri, ili kufikia hifadhi zote za mafuta katika eneo hilo, akisema kuwa hatua hiyo ingewakilisha utendaji bora.
Hata hivyo, wakosoaji wa ripoti hiyo wanasisitiza kuwa mapendekezo yake ni maoni tu, na kwamba mbinu bora tayari zipo. Kulingana na wafuasi wa mradi huo, ikiwa ni pamoja na walioajiriwa na mashirika ya serikali kama vile Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA), hatua za kuridhisha za kukabiliana nazo zilitambuliwa, na utekelezaji wake umekuwa ukiendelea bila kiulaini.
Pia wanadai kuwa awamu za utafutaji mafuta zilifanikiwa na kwamba hatua ya uzalishaji haijakumbana na changamoto zozote kwa sasa. Pia wanadai kuwa timu za wataalam zipo uwanjani ili kufuatilia na kuhakikisha upunguzaji iwapo kuna mabadiliko yoyote.

Inasalia kuamuliwa iwapo imani katika uwekezaji wa kutosha inafaa, kwani wasiwasi kama vile kutokuwepo kwa dhamira ya mfumo wa utupaji maji, maji taka na uchafu wa kuchimba visima vyote vinapendekeza matokeo mabaya katika eneo ambalo ni makazi ya wanyamapori fulani mahususi.
Watetezi wa Mazingira pia wanabainisha kwamba matumizi ya tope za uchimbaji wa kemikali ni hatari kwa mfumo ikolojia unaozunguka Ziwa Albert.
Zaidi ya hayo, kuna hofu kuwa mara tu uzalishaji wa mafuta unaanza, itakuwa vigumu kudhibiti maji asili ya dhoruba pamoja na kiasi kikubwa cha uchafu na taka, ali ambayo inaweza kuongeza hatari ya mifereji ya maji yenye haidrokaboni kutiririka hadi kwenye Mto Kamansinig na maeneo oevu yanayozinira.
Robert Agenonga ni mshauri maalum wa kimkakati kwa Watetezi wa Mazingira.
Picha ya bango: Korono ni mojawapo ya spishi za kipekee zinazotegemea Ziwa Albert nchini Uganda. Picha na Emilie Chen kupitia Flickr (CC BY-ND 2.0).
Maoni haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza hapa kwa lugha ya Kiingereza mnamo tarehe 24/10/2025